kiswahili

  

 

                                IDARA YA KISWAHILI
                                                            
         Somo la Kiswahili ni mojawapo wa masomo ya lazima katika mfumo ya 8-4-4 katika shule za upili. Hivyo basi wanafunzi hawana budi ila kujizatiti na kuhakikisha ya kuwa wanapata maki za juu katika somo hili.
         Hata hivyo somo hili limekumbwa na chandamoto si haba katika shule hii zimewemo matumizi ya sheng ambayo yameathiri wanafunzi sana. Uhaba wa walimu wa kutosha wa kuweza kuwahudumia wanafunzi vilivyo ni tatizo kwa idara hii, Pia baadhi ya vihana wameathiriwa na lugha zao za kwanza jambo linalowafanya kutotamka maneno visivyo na hivyo kutoandika lugha sanifu.
           Wanafunzi wengi hawaoendelei kusoma vitabu na magazeti ya Kiswahili ili wawe na uzoefu wa kuzungumza lugha sanifu. Haya yote hufanya wanafunzi kutojimudu vyema katika lugha hii.
             Isitoshe walimu wa idara hiii wameweka mikakati kabambe kuhakikisha ya kuwa wanafunzi wanaongea lugha sanifu. Hii ni kupitia kwa masomo ya maktaba ambayo huwapa wanafunzi fursa ya kusoma magazeti na vitabu vya hadidhi. Uandishi wa madarasa yote jambo ambalo bila shaka litasadia kuinua viwango vya Kiswahili shuleni.
             Idara hii ina walimu wanane wenye tajiriba ya kutosha na ni:
                                             
                                    Bi. Abung’ana-  Mkuu wa somo
                                     Bi.  Weswa  .C.
                                      Bw. Chanzu
Bw. Nyongesa
Bw. Oriendo
Bw. Amanya
Bw. Libibi
Bw.  Amayamu
           Natoa shukrani zangu za dhati kwa walimu wote wa idara hii kwa bidii zao za mchwa ambazo zimetufikisha mahali tulipo. Hata ingawa mwaka jana tulipata kiwango cha 8.200 katika matokeo ya K.C.S.E tuna matumaini makuu ya matokeo haya kuimarika zaidi mwaka huu kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhalifu. Asanteni.
Mkuu wa Idara ya Kiswahili
Bi. ..E. Abung’ana.

Home

WELCOME TO KAKAMEGA SCHOOL

 

School motto:    ’IN UNITY IS STRENGTH’

 

Vision:…

read more

Academics

click here to view kcse - 2010

read more